mtaka cha mvunguni kachutama

mtaka cha mvunguni kachukua kalamu kaandika

mtaka cha mvunguni lazima aende darasani kufunza

mtaka cha mvunguni lazima aende kazi ilipo

mtaka cha mvunguni sharti ainame

ukitaka nenda uchukue

ukitaka ng’ang’ana

ukitaka jieleze

ukitaka fanya juu chini kukipata

kwani ni kweli mtaka cha mvunguni sharti ainame

umekaa bure ukinena unataka

wataka kweli

ukitaka nenda ilipo

hata ukashindwa kunielewa

mtaka cha mvunguni sharti ainame

nilienda kuchukua

wakaniambia la!

juhudi zako hazionekani

ni kutaka tu wajua

sharti uiname

kwa kila unachokitaka

hata ikiwa ni mabadiliko

chakula, makao na mazao

bidii za mchwa zatakikana

kweni mtaka cha mvunguni sharti ainame

wacha kufukuza kuni utanuka moshi

fukuza ajira utanukia kazi

fukuza mali utaipata

fukuza chakula inukie

utakuwa umeinama

Advertisements